March 7, 2026

Bidhaa

HISA

AKIBA

  • Ni michango ambayo mwanachama anajiwekea katika akaunti yake mara kwa mara kwa ajili ya kukidhi mahitaji yake ya malengo aliyojiwekea kwa baadae.
  • Mwanachama anaweza kujiwekea michango hiyo kutoka kwenye mshahara wake au fedha taslimu isiyopungua 30,000/= kila mwezi ( kiasi ambacho kinaweza kubadilika kulingana na mahitaji ya wakati huo)
  • Mwanachama aliye na mkopo hatoruhusiwa kupunguza akiba zake chini zaidi ya madeni yake chamani.

 

FAIDA YA AKIBA

  1. Haina gharama za uendeshaji kwa mwanachama.
  2. Bidhaa hii humuwezesha mwanachama kufikia malengo kwa sababu huweza kuweka pesa yake kidogo kidogo kwa muda mrefu.
  3. Akiba hiyo humuwezesha mwanachama kukopa hadi mara 3 ya akiba yake aliyojiwekea kwa kuzingatia kanuni za mikopo.
  4. Bidhaa hii humuwezesha mwanachama kujenga tabia ya kujiwekea akiba mara kwa mara ( saving culture)
  5. Bidhaa hii inampa faida mwanachama ya 8% kwa mujibu wa sera ya Akiba kwa akiba ya kuanzia 500,000/=

AMANA

Ni mfumo wa kujiwekea pesa kwa ajili ya kukidhi haja mbalimbali za kidharura wakati wowote. Haina masharti ya kutoa notisi ya siku kadhaa za kuomba kuchukua amana yake, ni siku yoyote na saa yoyote.

 

FAIDA ZAKE:

  1. Mwanachama anaweza kuweka pesa na kuitoa muda huo huo bila kutoa notisi yoyote.
  2. Mwanachama anaweza kuweka pesa na kuitoa kwa kutumia simu yake ya mkononi kupitia Ura mobile.
  3.  Mwanachama atapata faida ya 9% kwa sasa kwa kiwango cha kuanzia 500,000/= zilizo kwenye akaunti yake.