Siku ya Makabidhiano ya uenyekiti wa Bodi tarehe 30 Disemba 2025, ambapo mwenyekiti mstaafu Balozi CP- Suzan S. Kaganda amemkabidhi CP - Tatu Rashid Jumbe aliyechaguliwa kuwa mjumbe na mwenyekiti wa Bodi ya Chama Novemba 28, 2025.
Washiriki wa Mafunzo Maalum ya Kuwajengea Uwezo wa Kiutendaji Wawakilishi Wa Ura Saccos wa Mikoa ya Kanda ya kati yaliyofunguliwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) George Katabazi tarehe 24-05-2025.
Wajumbe wa Bodi wa Ura Saccos pamoja na wawakilishi wakifuatilia mafunzo kwa kina katika elimu ya kuwajengea uwezo Wawakilishi wa kanda ya kati.
Mwakilishi wa Wilaya ya Hai D/SGT PAULINA K. MASHINA Akiuliza swali kwenye Mafunzo Maalum ya Kuwajengea Uwezo wa Kiutendaji Wawakilishi Wa Ura Saccos.
Mwakilishi wa Intel Kuu A/insp Hassan Hassan Akiuliza swali kwenye Mafunzo Maalum ya Kuwajengea Uwezo wa Kiutendaji Wawakilishi Wa Ura Saccos.
Balboa Daniel Moshi - ASP Afisa Mikopo wa Ura Saccos akiwasilisha mada ya Mikopo kwa wawakilishi wa Mikoa ya Kanda ya kati katika elimu ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji.
Julius Emanuel Mbise - SP Meneja wa Tawi la Ura Saccos Dodoma akiwasilisha mada ya Elimu ya fedha kwa wawakilishi wa Mikoa ya Kanda ya kati jijini Dodoma.
Washiriki wa Mafunzo Maalum ya Kuwajengea Uwezo wa Kiutendaji Wawakilishi Wa Ura Saccos wa Mikoa ya Kanda ya ziwa na Mikoa ya Kigoma na Katavi yaliyofunguliwa na afande, GIDEON H. MSUYA - SACP kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza tarehe 19-05-2025.
Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa Wa Mwanza GIDEON H. MSUYA - SACP akiwasisitiza washiriki wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo wa Kiutendaji wa mikoa ya Kanda ya Ziwa, Kigoma na Katavi wawe makini katika kufuatilia mafunzo hayo ili iwasaidie katika kwenda kuwahudumia wanachama katika himaya zao.
Afisa Mahusiano wa Ura Saccos RICHARD MUSSA BUSIMBA - SSP Akiwasilisha mada ya Uwelewa wa Chama kwa Wawakilishi walioshiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji mkoani Mwanza.
Washiriki wa Mafunzo Maalum ya Kuwajengea Uwezo wa Kiutendaji Wawakilishi Wa Ura Saccos wa Mikoa ya Kanda ya ziwa na Mikoa ya Kigoma na Katavi yaliyofunguliwa na afande, GIDEON H. MSUYA - SACP kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza tarehe 19-05-2025.
Daniel Robert Komba - A/Insp Mkaguzi wa Ndani wa Ura Saccos akiwasilisha mada ya Vihatarishi,udhibiti na ukaguzi wa ndani kwa wawakilishi wa mikoa ya kanda ya ziwa, Kigoma na Katavi.
Msei L. Mollel - A/Insp Akiwasilisha mada ya Tehama kwa wawakilishi wa mikoa ya kanda ya ziwa, Kigoma na Katavi walioshiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji.
Wachekeshaji wa FUTUHI
Tarehe 07.05.2025 URA SACCOS Ltd ilipokea Hati ya Pongezi kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora RICHARD ABWAO - SAC kwa kutambua mchango mkubwa unaotolewa na chama hicho kwa Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mh. Naitapwaki Tukai akikabidhi hati ya shukrani ambaye ametoa pongezi kwa URA SACCOS Ltd kwa kutoa misaada mbalimbali katika mkoa huo.
Meneja msaidizi wa Ura Saccos SSP Peter M. Msuya akimwelezea jambo Mh. Rais na Amri Jeshi Mkuu wa Jamhuri wa Muungano Wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan katika halfa ya Uzinduzi wa Benki ya UshirikaTanzania yaliyofanyika Jijini Dodoma Tarehe 27 na 28 April 2025
Siku ya Uzinduzi wa Benki ya UshirikaTanzania Tarehe 27 na 28 April 2025
Meneja msaidizi wa Ura Saccos SSP Peter M. Msuya akimwelezea jambo Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano Wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa katika halfa ya Uzinduzi wa Benki ya UshirikaTanzania yaliyofanyika Jijini Dodoma Tarehe 27 na 28 April 2025
Wajumbe wa Bodi na Wawakilishi wa PORTS SACCOS Kutoka nchini Kenya Waliotembelea URA SACCOS tarehe 16/04/2025 kwa ajili ya Ziara ya Kuja Kujifunza Mambo Mbalimbali Kutoka URA SACCOS.