March 7, 2026

omba kitambulisho

 

Maelekezo ya Kupiga Picha kwa Ajili ya Kitambulisho

a) Maelekezo sahihi ya namna ya kupiga picha kabla ya kuomba Kitambulisho kwenye mfumo:

  1. Kamera ya kawaida au ya Simu yenye uwezo angalau wa kuanzia megapixel 2.
  2. Picha ipigwe kwenye mwanga wa mchana bila flash na kivuli.
  3. Upigapo picha simama umbali wa futi 1 toka kwenye usuli (background) nyeupe au bluu.
  4. Piga picha ukiwa umevaa shati au blauzi ya kiraia.
  5. Simama wima ukiwa umeangalia kamera wakati wa upigaji picha.
  6. Usifumbe macho wakati wa kupigwa picha.
  7. Fumba mdomo na usitabasamu.

b) Picha zinazokubalika:

  1. Inaweza kuwa ya kawaida bila kufunika kichwa.
  2. Waweza kuvaa miwani ila isiwe mieusi inayofunika macho.
  3. Waweza vaa hijabu au baragashia.
  4. Usivae kapelo.

c) Muhimu:

Baada ya kupiga picha yako, chukua kalamu yako sasa na karatasi nyeupe na uandike sahihi yako vizuri. Kisha ipige picha sahihi hiyo kukiwa na mwanga mzuri.