
URA SACCOS imekamilisha taratibu za makabidhiano ya uenyekiti wa Bodi tarehe 30 Disemba 2025, ambapo mwenyekiti mstaafu Balozi CP- Suzan S. Kaganda amemkabidhi CP – Tatu Rashid Jumbe aliyechaguliwa kuwa mjumbe na mwenyekiti wa Bodi ya Chama Novemba 28, 2025.
Balozi kaganda aliteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe hivyo akajiuzulu nafasi ya ujumbe wa bodi na uenyekiti aliodumu nao tangu mwaka 2023.
CP Kaganda ameshukuru ushirikiano mkubwa wa Mlezi wa Chama afande CPF-IJP Camillus M. Wambura wakati akitekeleza majukumu yake kwa lengo la kuboresha ustawi wa watumishi katika Jeshi la Polisi na familia zao.
Aidha, CP Tatu ameahidi kuendeleza maono mazuri na mafanikio yaliyopatikana toka chama kilipoanzishwa mwaka 2006 na pia atashirikiana na Bodi, watendaji, na wanachama ili kuiboresha zaidi URA SACCOS kwa kuzingatia kuwa yeye kama kamishna wa Utawala na menejimenti ya rasilimali watu, ndiye msimamizi mkuu wa ustawi wa watumishi katika Jeshi.
Makabidhiano hayo yamefanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dodoma na kushuhudiwa na afisa ushirika Mr Haidar Abdulkhakim.



1 thought on “MAKABIDHIANO YA MADARAKA”