TUZO mbalimbali zimetolewa katika Siku ya Ushirika Duniani ambayo imeunganika na maadhimisho ya sherehe ya Nanenane Jijini Dodoma.
URA SACCOS LTD imefanikiwa kupata Tuzo pamoja na Cheti cha Chama Bora katika utendaji eneo la Utawala Bora na kufuata sheria (compliance).
Tuzo pamoja na cheti vimetolewa na Shirikisho la Vyama vya Ushirika Nchini (TFC).
Tuzo hizo zilitolewa tarehe 03/08/2025 ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. KASSIM MAJALIWA.

