Habari zote

MIKUTANO

URA SACCOS yashiriki mafunzo na mkutano wa ACCOSCA nchini Kenya

Mkutano wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Afrika umefanyika Naivasha ukishirikisha nchi 44, Tanzania ikiwakilishwa na wajumbe wapatao 70.

URASACCOS Admin

Mafunzo na Mkutano wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Afrika (ACCOSCA) umefanyika nchini Kenya katika mji wa Naivasha. Lengo lilikuwa kujenga uwezo wa kusimamia uendeshaji bora wa vyama, kubadilishana uzoefu katika huduma na bidhaa, na kubaini maeneo yanayoweza kushawishi maboresho ya sera za nchi.

Nchi 44 zilishiriki, ambapo Tanzania iliwakilishwa na wajumbe wapatao 70 kutoka vyama na wadau mbalimbali. URA SACCOS ilikuwa miongoni mwa vyama shiriki, ikiwa na baadhi ya wajumbe wa Bodi, Kamati ya Usimamizi na watendaji. Kilele cha mafunzo na mkutano huo kilikuwa tarehe 11 Oktoba 2024.

Picha zaidi

Imechapishwa pia kwenye Instagram

Shiriki: