Akiba na hisa

Akiba yako ya kila mwezi hukatwa moja kwa moja kwenye mshahara wako. Ndiyo msingi wa uwezo wako wa kukopa, na hisa zako hulipwa gawio.

  • 01

    Akiba ya Kila Mwezi

    Mchango wako wa kila mwezi unakatwa moja kwa moja kwenye mshahara (kanuni ya makato 667) na kuongeza uwezo wako wa kukopa.

    • Makato ya moja kwa moja kwenye mshahara — hakuna kusahau
    • Akiba ndiyo msingi wa mkopo: unaweza kukopa hadi mara 3 ya akiba yako
    • Unaweza kubadilisha kiasi cha mchango wako (fomu tawini au kupitia mwakilishi wako)
    Maelezo zaidi
  • 02

    Hisa

    Umiliki wako katika ushirika. Hisa hununuliwa mara moja au kwa awamu na hulipwa gawio kadri ushirika unavyopata ziada.

    • Kila mwanachama anamiliki hisa katika ushirika
    • Gawio kulingana na uamuzi wa Mkutano Mkuu
    • Angalia hisa zako kwa URA Mobile (*149*32#)
    Maelezo zaidi
  • 03

    Amana

    Weka fedha za ziada kwa hiari juu ya akiba yako ya kila mwezi, kwa control number ya akaunti yako.

    • Malipo kwa control number — benki au simu
    • Taarifa ya akaunti kwa URA Mobile au barua pepe
    Maelezo zaidi

Weka akiba, hisa na amana, angalia salio na toa amana kwa simu ukitumia URA Mobile (*149*32#). Jinsi ya kutumia URA Mobile

Unaweza kubadilisha kiasi cha akiba yako ya kila mwezi wakati wowote; mabadiliko huanza mwezi unaofuata wa mshahara. Amana za ziada hulipwa kwa control number ya akaunti yako. info@urasaccos.co.tz