MATUKIO
Askari wa STPU Arusha wapewa elimu ya uwekezaji na uwekaji akiba
Meneja wa URA SACCOS Mkoa wa Arusha, CPL Chiunda David, amewahimiza askari kutumia fursa za chama zikiwemo hisa na kufuatilia mwenendo wa akiba zao.
URASACCOS Admin
Askari wa Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo Nchini (STPU) mkoani Arusha, tarehe 15 Septemba 2026, wamepewa elimu juu ya faida ya uwekezaji pamoja na kuweka akiba kwa maendeleo yao. Elimu hiyo imetolewa na Meneja wa URA SACCOS Mkoa wa Arusha, CPL Chiunda David.
CPL Chiunda amesema ni vyema askari hao wakazitumia vyema fursa zinazopatikana katika SACCOS, ikiwemo ununuzi wa vipande vya hisa vitakavyochagiza maendeleo yao kiuchumi, pamoja na kuwa na utamaduni wa kufuatilia mwenendo wa akiba zao katika mfuko wa chama.
Aidha, amewakumbusha askari hao haki na wajibu wao katika maendeleo ya chama, na kuwasisitiza kujenga utamaduni wa kujiongezea maarifa katika nyanja za uwekezaji na uwekaji akiba.
Picha zaidi
Imechapishwa pia kwenye Instagram

