Habari zote

MATUKIO

Mwenyekiti wa Bodi akutana na askari na watumishi wa Dar es Salaam kutoa elimu ya chama

Katika ukumbi wa Police Officers Mess, Oyster Bay, CP Suzan Kaganda na wataalamu wa URA SACCOS wametoa elimu ya huduma za chama na matumizi sahihi ya fedha.

URASACCOS Admin

Mwenyekiti wa Bodi ya URA SACCOS, ambaye pia ni Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu ndani ya Jeshi la Polisi, CP Suzan Kaganda, tarehe 15 Juni 2024 amekutana na makamanda, maafisa, wakaguzi, askari wa vyeo mbalimbali na watumishi raia wa Jiji la Dar es Salaam katika ukumbi wa Police Officers Mess, Oyster Bay.

Lengo lilikuwa kuwapa elimu na uelewa zaidi wa chama chao, sambamba na matumizi sahihi ya rasilimali fedha. Wataalamu wa URA SACCOS Ltd walitoa mada mbalimbali juu ya huduma zinazotolewa na chama na faida zake.

Katika baraza hilo, CP Kaganda pia alitoa maelekezo ya Makao Makuu kwa makamanda wa mikoa na vikosi waliohudhuria kuhusu usimamizi wa mifumo ya kiutendaji na nidhamu ndani ya Jeshi, pamoja na kutatua changamoto za askari zinapowasilishwa.

Picha zaidi

Imechapishwa pia kwenye Instagram

Shiriki:
Mwenyekiti wa Bodi akutana na askari na watumishi wa Dar es Salaam kutoa elimu ya chama | URASACCOS