HAFLA
URA SACCOS yapewa hati ya pongezi na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora
Hati hiyo inatambua mchango mkubwa wa chama kwa Jeshi la Polisi, na imetolewa kwenye sherehe za kuwapongeza askari waliofanya vizuri mwaka 2024.
URASACCOS Admin
Tarehe 7 Mei 2025 URA SACCOS Ltd imepokea hati ya pongezi kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao, katika sherehe za kuwapongeza maafisa, wakaguzi na askari waliofanya vizuri zaidi kwa mwaka 2024 mkoani Tabora.
Hati hiyo imetokana na kutambua mchango mkubwa unaotolewa na chama kwa Jeshi la Polisi.
Mgeni rasmi katika sherehe hiyo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Paul Matiko Chacha, aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Mhe. Naitapwaki Tukai, ambaye ametoa pongezi kwa URA SACCOS Ltd kwa misaada mbalimbali iliyotolewa mkoani humo.
Picha zaidi
Imechapishwa pia kwenye Instagram

