Habari zote
MATUKIO
URA SACCOS yashiriki maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Ushirika wa Akiba na Mikopo (ICUD 2024)
Kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mbugani, Mwanza, banda la URA SACCOS limetembelewa na Mrajis wa Vyama vya Ushirika, Dkt. Benson Ndiege.
URASACCOS Admin
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Ushirika wa Akiba na Mikopo (ICUD 2024) yamefanyika kitaifa jijini Mwanza katika viwanja vya Shule ya Msingi Mbugani. URA SACCOS Ltd imeshiriki kwenye maonesho hayo kwa kuonesha bidhaa na huduma zake.
Tarehe 23 Oktoba 2024 banda letu limetembelewa na Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Dkt. Benson Ndiege, ikiwa ni kuelekea kilele cha maonesho hayo tarehe 24 Oktoba 2024.
Picha zaidi
Imechapishwa pia kwenye Instagram

