Habari zote

MIKUTANO

Maazimio ya Mkutano Mkuu wa 13 uliofanyika Mbeya, 29 Oktoba 2021

Riba ya mkopo imepunguzwa kutoka 8.1% hadi 7.5% kwa mwaka kuanzia Januari 2022, na mwaka 2022 umetangazwa kuwa mwaka wa kuhamasisha akiba, amana na hisa.

URASACCOS Admin

Mkutano Mkuu wa 13 wa URA SACCOS ulifanyika tarehe 29 Oktoba 2021 mkoani Mbeya na kuazimia yafuatayo:

  • Kupunguza riba ya mkopo kutoka 8.1% hadi 7.5% kwa mwaka kuanzia Januari 2022, na akiba na amana kulipwa riba ya 5.5% kwa mwaka.
  • Kuendelea kutoa elimu ya ushirika kwa watendaji, wawakilishi na wanachama.
  • Kuendelea kukamilisha na kuimarisha matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika huduma za chama.
  • Bodi na menejimenti wafanye utafiti wa bidhaa mpya za kuongeza mapato, kwa mfano Toto Akiba na wakala wa bima.
  • Kuwafikia wasio wanachama na kuwapa elimu ya faida za uanachama.
  • Mwaka 2022 uwe mwaka wa uhamasishaji mkubwa wa kuongeza akiba, amana na hisa, ili Mkutano Mkuu ujao uweze kuamua kuhusu kuongeza muda wa marejesho ya mkopo.
  • Hisa za chama katika NMB na Vodacom ziuzwe kutokana na faida ndogo, na fedha hizo zipelekwe kwenye mikopo ya wanachama.
Shiriki: