Habari zote
MIKUTANO
Maazimio ya Mkutano Mkuu wa 15 uliofanyika Morogoro, 19 na 20 Oktoba 2023
Riba ya mkopo imeshuka hadi 12% kwa salio linalopungua, kiingilio kimepanda, na wanachama wataelimishwa kutumia URA Mobile.
URASACCOS Admin
Mkutano Mkuu wa 15 wa URA SACCOS ulifanyika tarehe 19 hadi 20 Oktoba 2023 mkoani Morogoro na kuazimia yafuatayo:
- Kulinda na kuongeza ukwasi wa chama: kiingilio cha mwanachama mpya kipande kutoka TZS 10,000 hadi TZS 20,000, na sehemu ya posho ya kujikimu ya vikao vya wanachama iwekwe kwenye akaunti zao za amana ili wapate huduma za URA Mobile.
- Kulingana na takwa la kisheria, riba ya mkopo ishuke kutoka 7.5% hadi 6.6% kwa njia ya mnyoofu (straight line), sawa na 12% kwa njia ya salio linalopungua (reducing balance).
- Wanachama waelimishwe na kuhamasishwa kutumia mfumo wa kidijitali wa URA Mobile Money.
- Ufanyike utafiti wa ufanisi wa bidhaa za chama, pamoja na bidhaa na huduma mpya zitakazowanufaisha wanachama.
- Elimu ya kuongeza akiba, hisa na amana iendelee, na elimu kwa wawakilishi na watendaji itolewe kikanda.
- Kupunguza mikopo chechefu ya taslimu: mwakilishi wa mkopaji afuatilie marejesho kwa wakati, na mdhamini ajaze fomu maalum ya kisheria ya kukubali kubeba deni pindi mkopaji atashindwa kurejesha.
