HAFLA
Hafla ya makabidhiano ya Bodi: CP Suzan Kaganda apokea uenyekiti kutoka kwa CP Benedict Wakulyamba
Hafla imefanyika Police Officers Mess, Dar es Salaam, tarehe 9 Novemba 2023, ikitanguliwa na semina elekezi kwa wajumbe wapya wa Bodi.
URASACCOS Admin
Mwenyekiti wa Bodi ya URA SACCOS Ltd, CP Suzan Kaganda, amekabidhiwa rasmi jukumu la kuiongoza Bodi na aliyekuwa Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, CP Benedict Wakulyamba, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii. Hafla hiyo ilifanyika tarehe 9 Novemba 2023 katika Police Officers Mess, Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na wajumbe wa Bodi waliochaguliwa na waliomaliza muda wao, wajumbe wa Kamati ya Usimamizi na Menejimenti ya chama.
Kabla ya makabidhiano, wajumbe wa Bodi waliochaguliwa walipewa semina elekezi na Maafisa Ushirika kutoka Jiji la Dar es Salaam, iliyolenga kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao ndani ya chama.
Katika hafla hiyo tuzo ya uongozi bora ilitolewa kwa Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, na vyeti vya pongezi kwa wajumbe wa Bodi waliomaliza muda wao, ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wao mkubwa katika kukiongoza chama vizuri.
Picha zaidi
Imechapishwa pia kwenye Instagram

