Habari zote

MIKUTANO

Mkutano Mkuu wa 14 wafunguliwa Mwanza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani

Mhe. Jumanne Sagini amepongeza URA SACCOS kwa huduma bora na tuzo ya hati safi bora kati ya vyama 1,849 vilivyokaguliwa mwaka 2021.

URASACCOS Admin

Mkutano Mkuu wa 14 wa URA SACCOS Ltd wa mwaka 2022 umefunguliwa tarehe 28 Oktoba 2022 jijini Mwanza, katika ukumbi wa Rock City Mall, na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Jumanne Sagini (Mb).

Akifungua mkutano, Mhe. Sagini ameipongeza URA SACCOS kwa kutoa huduma bora kwa wanachama wake, kwa kuendelea kupata tuzo mbalimbali za chama bora cha ushirika, na kwa tuzo ya hati safi bora kati ya vyama 1,849 vilivyokaguliwa na Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika Tanzania mwaka 2021. Amewataka wajumbe kuendelea kuongeza ubunifu ili kukuza mtaji wa chama na kuleta faida zaidi.

Mwenyekiti wa Bodi, CP Benedict Wakulyamba, alisema URA SACCOS imeendelea kutoa mikopo yenye riba nafuu kuliko taasisi nyingine za kifedha, pamoja na mkono wa pole kwa wanachama waliolazwa hospitali kwa siku 30 au zaidi, rambirambi kwa familia zilizofiwa na mwanachama, mwenza au mtoto, na msaada kwa mwanachama aliyeumia au kupata maafa akiwa kazini.

Picha zaidi

Imechapishwa pia kwenye Instagram

Shiriki:
Mkutano Mkuu wa 14 wafunguliwa Mwanza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani | URASACCOS