Habari zote

MIKUTANO

Mkutano Mkuu wa 16 wafanyika Mwanza chini ya kaulimbiu "Wekeza kwa Maendeleo Endelevu"

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Mhe. Ally Gugu, amepongeza chama kwa tuzo na hati safi mfululizo mbele ya wawakilishi na watendaji zaidi ya 200.

URASACCOS Admin

Tarehe 30 Oktoba 2024 Mkutano Mkuu wa 16 wa URA SACCOS Ltd umefanyika jijini Mwanza katika ukumbi wa Rock City Mall, ukiongozwa na kaulimbiu "Wekeza kwa Maendeleo Endelevu". Mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Ally Gugu.

Akizungumza na wawakilishi na watendaji wa URA SACCOS zaidi ya 200 waliotoka Tanzania Bara na Zanzibar, mgeni rasmi amekipongeza chama kwa kupata tuzo mbalimbali, kuendelea kuwa chama bora cha ushirika wa akiba na mikopo, na kupata hati safi mfululizo kutoka kwa mkaguzi wa nje.

Mhe. Gugu alisema chama kimechangia katika mzunguko wa fedha na ukuaji wa pato la Taifa, ikiashiria kuwa sekta ya ushirika nchini, ikisimamiwa na kuimarishwa kwa weledi, inaweza kuwa miongoni mwa sekta zinazoongoza katika ukuaji wa uchumi.

Picha zaidi

Imechapishwa pia kwenye Instagram

Shiriki:
Mkutano Mkuu wa 16 wafanyika Mwanza chini ya kaulimbiu "Wekeza kwa Maendeleo Endelevu" | URASACCOS