Habari zote

MATUKIO

URA SACCOS yatoa vifaa vya kufundishia Chuo cha Taaluma ya Polisi (DPA)

Vifaa vya kukuza sauti kwa madarasa makubwa na mihadhara ya wazi vimekabidhiwa tarehe 18 Machi 2023 kwa mujibu wa msingi wa saba wa ushirika.

URASACCOS Admin

Jumamosi tarehe 18 Machi 2023 URA SACCOS imekabidhi vifaa vya kufundishia katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA). Vifaa hivyo ni maalumu kwa kukuza sauti na kuboresha usikivu katika madarasa makubwa na mihadhara ya maeneo ya wazi (PA system).

Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya uongozi wa chama, Meneja Mkuu Msaidizi SSP Peter Mark Msuya alieleza kuwa jambo hilo limefanyika kwa kuzingatia msingi wa saba wa ushirika unaovitaka vyama kurudisha sehemu ya faida kwa jamii, hususani katika maeneo ya elimu, afya na maji.

Mkuu wa Chuo, Dkt. SACP Lazaro Mambosasa, amesema vifaa hivyo vitakuwa msaada mkubwa kwani chuo kina idadi kubwa ya wanafunzi katika mafunzo ya uongozi wa Polisi, stashahada na cheti. Mwenyekiti wa Bodi, CP Benedict Wakulyamba, amesema Bodi itaendelea kuhakikisha chama kinaimarika huku kikifuata sheria, kanuni na miongozo ya ushirika, kwani hiyo ndiyo silaha kuu ya kumhakikishia mwanachama usalama wa fedha zake.

Picha zaidi

Imechapishwa pia kwenye Instagram

Shiriki: