Habari zote
HAFLA
URA SACCOS mshindi wa kwanza kitaifa: chama bora cha ushirika wa akiba na mikopo 2022
Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe amekabidhi tuzo ya chama bora na tuzo ya banda bora la maonesho kwenye Siku ya Ushirika Duniani, Tabora.
URASACCOS Admin
URA SACCOS Ltd imepata tuzo ya ushindi wa Chama Bora cha Ushirika wa Akiba na Mikopo mwaka 2022, pamoja na tuzo ya banda bora la maonesho ya Siku ya Ushirika Duniani (SUD). Tuzo zimetolewa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein M. Bashe (Mb), tarehe 2 Julai 2022 mkoani Tabora, na kupokelewa na mjumbe wa Bodi ya chama, ACP Festo C. Ngwenuki.
Mwenyekiti mstaafu wa Bodi ya URA SACCOS Ltd na mwanachama hai, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias E. M. Andengenye (CP), aliungana na wana-URA SACCOS kusherehekea tuzo hizo.
Picha zaidi
Imechapishwa pia kwenye Instagram

