TAARIFA
Rasilimali za SACCOS Nchini kwa Mwaka 2025 (Taarifa ya TCDC)
Usalama wa Raia SACCOS (URA SACCOS) inaongoza kwa rasilimali nchini mwaka 2025 kwa TZS bilioni 201.84, ukuaji wa 23.81%, kwa mujibu wa taarifa ya mwaka ya TCDC.

Jedwali likionyesha ukubwa wa rasilimali za Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo kwa mwaka 2025 kama ilivyotolewa kwenye taarifa ya mwaka ya Tume ya Maendeleo ya vyama vya ushirika nchini (TCDC) iliyozinduliwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dr. Mwigulu Lameck Nchemba, tarehe 15 Oktoba 2026.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Usalama wa Raia SACCOS Ltd (URA SACCOS) imeshika nafasi ya kwanza kwa rasilimali za TZS bilioni 201.84 mwaka 2025, kutoka TZS bilioni 163.03 mwaka 2024, ikiwa ni ukuaji wa asilimia 23.81.
#TunakuzaUstawiWetu #TunalindaJamiiYetu

