Habari zote

TAARIFA

Tangazo la mnada usio wazi wa uuzaji wa mali chakavu

Menejimenti ilitangaza mnada kwa wanachama pekee wa gari, kompyuta na samani zilizoidhinishwa kufutwa katika Daftari la Mali za Kudumu. Ofa zilipokelewa hadi tarehe 30 Septemba 2026.

URASACCOS Admin

Tarehe 3 Septemba 2026 Menejimenti ya URA SACCOS LTD ilitangaza mnada usio wazi kwa njia ya barua za ofa, kwa ajili ya kuuza mali chakavu zilizoidhinishwa kufutwa katika Daftari la Mali za Kudumu. Mnada uliwahusu wanachama hai wa chama pekee.

Mali zilizouzwa ni pamoja na:

  • Gari aina ya Toyota Alphard (2004)
  • Kompyuta za mezani, monita, UPS, printa, skana na kompyuta mpakato
  • Router na kiyoyozi
  • Viti na meza za ofisi

Mali hizo zilikuwa Makao Makuu na kwenye matawi ya Kigoma, Mwanza, Mbeya, Dodoma, Tanga na Zanzibar, na ziliuzwa katika hali zilivyo na mahali zilipo. Wawakilishi, wajumbe wa Bodi na Kamati ya Usimamizi, watendaji na viongozi wa Menejimenti hawakuruhusiwa kushiriki.

Muda wa kupokea ofa ulimalizika tarehe 30 Septemba 2026, saa 9:00 alasiri.

Shiriki:
Tangazo la mnada usio wazi wa uuzaji wa mali chakavu | URASACCOS