HAFLA
Ni URA SACCOS tena: tuzo ya SACCOS bora kwa vyama vya waajiriwa kundi B
Tuzo ya TCDC imetolewa Arusha tarehe 29 Septemba 2025 wakati wa uzinduzi wa taarifa ya mwaka ya utendaji wa SACCOS nchini.
URASACCOS Admin
URA SACCOS imeibuka mshindi na kupata tuzo ya SACCOS bora katika vyama vinavyohudumia waajiriwa nchini, kundi B. Tuzo hizo zimeandaliwa na Tume ya Maendeleo ya Vyama vya Ushirika nchini (TCDC), ambayo ndiyo msimamizi wa vyama vya ushirika.
Tuzo imetolewa tarehe 29 Septemba 2025 jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa Taarifa ya Mwaka ya Utendaji wa Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo nchini. Katika kuwania tuzo hizo, TANESCO SACCOS na Hazina SACCOS ziliingia tatu bora.
Aidha, taarifa hizo za mwaka 2024 zimeonesha URA SACCOS inaongoza kwa rasilimali (assets) na mtaji tete (core capital), ikifuatiwa na Ngome SACCOS.
Picha zaidi
Imechapishwa pia kwenye Instagram

