HAFLA
URA SACCOS yapata tuzo ya SACCOS bora kwa vyama daraja B vya makazini, ICUD 2023
Vigezo vilikuwa hati safi ya ukaguzi, kujiendesha kwa mtaji wa ndani na kuwasilisha taarifa kwa wakati. Chama pia kimeshika nafasi ya pili kwa banda bora la maonesho.
URASACCOS Admin
Tarehe 26 Oktoba 2023 URA SACCOS imepata tuzo ya kuwa SACCOS bora kwa vyama daraja B vya makazini. Tuzo hiyo imetolewa katika hitimisho la maadhimisho ya Siku ya Ushirika wa Akiba na Mikopo Duniani (ICUD) yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza.
Miongoni mwa vigezo vilivyotumika ni hati safi ya ukaguzi wa hesabu, uwezo wa kujiendesha kwa kutumia mtaji wa ndani, na kuwasilisha kwa wakati taarifa za chama katika mfumo wa usimamizi. Vilevile URA SACCOS imepata ushindi wa pili wa banda bora la maonesho.
Tuzo ilikabidhiwa na mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Balandya M. Elikana, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kwa Meneja Msaidizi wa URA SACCOS.
Picha zaidi
Imechapishwa pia kwenye Instagram

