Habari zote

HAFLA

Tuzo na cheti cha utawala bora kutoka Shirikisho la Vyama vya Ushirika (TFC)

Katika Siku ya Ushirika Duniani iliyoungana na Nane Nane 2025 Dodoma, URA SACCOS imetunukiwa tuzo ya chama bora katika utawala bora na kufuata sheria.

URASACCOS Admin

Tuzo mbalimbali zimetolewa katika maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyoungana na sherehe za Nane Nane jijini Dodoma. URA SACCOS Ltd imefanikiwa kupata tuzo pamoja na cheti cha chama bora katika utendaji, eneo la utawala bora na kufuata sheria (compliance).

Tuzo na cheti vimetolewa na Shirikisho la Vyama vya Ushirika nchini (TFC) tarehe 3 Agosti 2025, mgeni rasmi akiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.

Picha zaidi

Imechapishwa pia kwenye Instagram

Shiriki:
Tuzo na cheti cha utawala bora kutoka Shirikisho la Vyama vya Ushirika (TFC) | URASACCOS