Habari zote

MATUKIO

URA SACCOS yapokea ugeni kutoka MSONKHO SACCOS ya Malawi

Viongozi wa SACCOS ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato ya Malawi walikuja kujifunza na kubadilishana uzoefu katika uendeshaji wa vyama vya ushirika wa kifedha.

URASACCOS Admin

Jumanne tarehe 6 Agosti 2024 URA SACCOS ilitembelewa na viongozi wa MSONKHO SACCOS, chama cha watumishi wa Mamlaka ya Mapato kutoka nchini Malawi. Wageni walikuja kujifunza na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya uendeshaji wa vyama vya ushirika wa kifedha.

Katika mazungumzo na Menejimenti ya URA SACCOS walieleza kuwa chama chao bado ni kichanga, kwani kilianzishwa Desemba 2023, hivyo walikuja kujifunza kutoka URA SACCOS, mojawapo ya SACCOS kubwa nchini Tanzania.

Wageni waliambatana na viongozi wawili wa TRA SACCOS, waliokuwa wenyeji wao katika kipindi chote cha ziara yao nchini.

Picha zaidi

Shiriki: