Habari zote

MATUKIO

Rais Dkt. Samia na Waziri Mkuu watembelea banda la URA SACCOS kwenye uzinduzi wa Benki ya Ushirika

URA SACCOS imeshiriki uzinduzi wa Benki ya Ushirika Tanzania (CBT) jijini Dodoma tarehe 27 na 28 Aprili 2025 kama chama cha ushirika na mwanahisa wa benki hiyo.

URASACCOS Admin

Uzinduzi wa Benki ya Ushirika Tanzania (CBT) umefanyika jijini Dodoma tarehe 27 na 28 Aprili 2025, ukijumuisha maonesho na makongamano, na kuhitimishwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuzindua rasmi benki hiyo tarehe 28 Aprili.

Kabla ya uzinduzi, Mheshimiwa Rais alitembelea banda la URA SACCOS Ltd akiongozana na Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb), na kujionea huduma na bidhaa zitolewazo pamoja na kusikia matarajio ya wanaushirika kutoka katika benki.

Siku ya kwanza, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akiongozana na Waziri wa Kilimo, naye alitembelea banda la URA SACCOS. URA SACCOS Ltd inashiriki uzinduzi huo kama chama cha ushirika na mwanahisa/mmiliki wa Benki ya Ushirika Tanzania.

Picha zaidi

Imechapishwa pia kwenye Instagram

Shiriki: