MATUKIO
URA SACCOS yakabidhi vifaa tiba na kompyuta vya TZS milioni 40.4 kwa Jeshi la Polisi
Vifaa tiba kwa zahanati za Kunduchi na Simiyu, na kompyuta 12 kwa vyuo vya ufundi stadi vya Polisi Ujenzi na Bohari Kuu.
URASACCOS Admin
Tarehe 22 Agosti 2022 URA SACCOS imekabidhi vifaa tiba pamoja na kompyuta kwa vikosi vya Jeshi la Polisi Tanzania. Vifaa tiba ni kwa ajili ya Zahanati ya Jeshi iliyopo Kunduchi, Dar es Salaam, na Zahanati ya Polisi Mkoa wa Simiyu. Kompyuta 12 zilizotolewa ni kwa ajili ya vyuo vya ufundi stadi vilivyopo Kikosi cha Polisi Ujenzi na Bohari Kuu ya Jeshi la Polisi.
Akikabidhi katika hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya URA SACCOS jijini Dar es Salaam, ACP Festo Christopher Ngwenuki, mjumbe wa Bodi, amesema vifaa vyote hivyo vina thamani ya TZS 40,361,000, ikiwa ni kutimiza takwa la kurudisha faida kwa jamii inayowazunguka.
Mkuu wa Kikosi cha Afya ACP Hussen Yahaya, Mkuu wa Kikosi cha Ujenzi ACP Fadhili Ishekazoba na Mboharia Mkuu ACP Moses Mziray wamekishukuru chama kwa msaada huo uliokuja wakati muafaka, wakisema kompyuta zitawasaidia vijana kupata ujuzi wa kujiajiri, na vifaa tiba vitawatibu askari, familia zao na wananchi waishio jirani na zahanati hizo.
Picha zaidi
Imechapishwa pia kwenye Instagram

