MATUKIO
Meneja Mkuu amtembelea IGP mstaafu Said Mwema kuelekea miaka 20 ya URA SACCOS
ACP Kim Onai Mwemfula amekutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu mkoani Kilimanjaro kupata tathmini na uzoefu wake kuelekea maadhimisho ya miaka 20 ya chama.
URASACCOS Admin
Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Kim Onai Mwemfula, ambaye ni Meneja Mkuu wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Usalama wa Raia (URA SACCOS), tarehe 17 Septemba 2026 mkoani Kilimanjaro amemtembelea Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu, IGP Said Mwema.
Lengo la ziara hiyo lilikuwa kupata tathmini na mchango wa uzoefu wake kuelekea maadhimisho ya miaka 20 ya URA SACCOS tangu kuanzishwa kwake. IGP Mwema anatambulika kwa ubunifu wake wa kuanzisha chama hiki ambacho kimeendelea kuweka ustawi bora kwa askari na watumishi wa Jeshi la Polisi.
Picha zaidi
Imechapishwa pia kwenye Instagram

