Habari na matukio
Taarifa kwa wanachama, hafla, mikutano mikuu na matukio ya ushirika.
2HAFLA
URA SACCOS yatunukiwa tuzo ya chama bora cha ushirika wa fedha kwa SACCOS za waajiriwa
Tuzo imetolewa na Jukwaa la Ushirika Mkoa wa Dar es Salaam tarehe 20 Mei 2026 na kukabidhiwa na Mrajis wa Vyama vya Ushirika, Dkt. Benson Ndiege.
4HAFLA
CP Tatu Rashid Jumbe apokea uenyekiti wa Bodi kutoka kwa Balozi CP Suzan Kaganda
Makabidhiano yamefanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dodoma tarehe 30 Desemba 2025 baada ya CP Kaganda kuteuliwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe.
2HAFLA
Ni URA SACCOS tena: tuzo ya SACCOS bora kwa vyama vya waajiriwa kundi B
Tuzo ya TCDC imetolewa Arusha tarehe 29 Septemba 2025 wakati wa uzinduzi wa taarifa ya mwaka ya utendaji wa SACCOS nchini.
2HAFLA
Tuzo na cheti cha utawala bora kutoka Shirikisho la Vyama vya Ushirika (TFC)
Katika Siku ya Ushirika Duniani iliyoungana na Nane Nane 2025 Dodoma, URA SACCOS imetunukiwa tuzo ya chama bora katika utawala bora na kufuata sheria.
3HAFLA
URA SACCOS yapewa hati ya pongezi na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora
Hati hiyo inatambua mchango mkubwa wa chama kwa Jeshi la Polisi, na imetolewa kwenye sherehe za kuwapongeza askari waliofanya vizuri mwaka 2024.
2HAFLA
URA SACCOS yajinyakulia tuzo ya SACCOS bora mahali pa kazi
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Juma Zubery Omella, amekabidhi tuzo ya TCDC kwa Meneja Mkuu ACP Kim O. Mwemfula kwenye uzinduzi wa taarifa ya utendaji wa SACCOS 2023.
5HAFLA
Tuzo nne kwa URA SACCOS kwenye kilele cha Siku ya Ushirika Duniani 2024, Tabora
Naibu Waziri Mkuu Dkt. Dotto Biteko amekabidhi tuzo za chama bora cha ushirika wa kifedha, mtaji mkubwa daraja B, kurudisha kwa jamii na udhamini wa SUD 2024.
5HAFLA
Hafla ya makabidhiano ya Bodi: CP Suzan Kaganda apokea uenyekiti kutoka kwa CP Benedict Wakulyamba
Hafla imefanyika Police Officers Mess, Dar es Salaam, tarehe 9 Novemba 2023, ikitanguliwa na semina elekezi kwa wajumbe wapya wa Bodi.
4HAFLA
URA SACCOS yapata tuzo ya SACCOS bora kwa vyama daraja B vya makazini, ICUD 2023
Vigezo vilikuwa hati safi ya ukaguzi, kujiendesha kwa mtaji wa ndani na kuwasilisha taarifa kwa wakati. Chama pia kimeshika nafasi ya pili kwa banda bora la maonesho.
