Habari na matukio
Taarifa kwa wanachama, hafla, mikutano mikuu na matukio ya ushirika.
4MATUKIO
URA Mobile yazinduliwa: huduma za chama kwenye simu saa 24
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Jumanne Sagini amepongeza matumizi ya TEHAMA wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kidijitali wa URA SACCOS tarehe 30 Septemba 2023.
2HAFLA
URA SACCOS mshindi kati ya SACCOS za majeshi ya ulinzi na usalama; cheti chatolewa na Gavana wa BoT
Gavana wa Benki Kuu, Bw. Emmanuel Tutuba, amekabidhi cheti kwenye uzinduzi wa taarifa ya utendaji wa SACCOS Tanzania jijini Mwanza.
4HAFLA
Ni URA SACCOS tena: chama bora cha ushirika wa kifedha kwa mwaka wa tatu mfululizo
Kwenye kilele cha Siku ya Ushirika Duniani 2023 mjini Tabora, Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe amekabidhi tuzo kwa Mwenyekiti wa Bodi CP Benedict Wakulyamba.
3MATUKIO
URA SACCOS yatoa vifaa vya kufundishia Chuo cha Taaluma ya Polisi (DPA)
Vifaa vya kukuza sauti kwa madarasa makubwa na mihadhara ya wazi vimekabidhiwa tarehe 18 Machi 2023 kwa mujibu wa msingi wa saba wa ushirika.
5MIKUTANO
Mkutano Mkuu wa 14 wafunguliwa Mwanza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani
Mhe. Jumanne Sagini amepongeza URA SACCOS kwa huduma bora na tuzo ya hati safi bora kati ya vyama 1,849 vilivyokaguliwa mwaka 2021.
5MATUKIO
URA SACCOS yakabidhi vifaa tiba na kompyuta vya TZS milioni 40.4 kwa Jeshi la Polisi
Vifaa tiba kwa zahanati za Kunduchi na Simiyu, na kompyuta 12 kwa vyuo vya ufundi stadi vya Polisi Ujenzi na Bohari Kuu.
4HAFLA
URA SACCOS mshindi wa kwanza kitaifa: chama bora cha ushirika wa akiba na mikopo 2022
Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe amekabidhi tuzo ya chama bora na tuzo ya banda bora la maonesho kwenye Siku ya Ushirika Duniani, Tabora.
MIKUTANO
Maazimio ya Mkutano Mkuu wa 13 uliofanyika Mbeya, 29 Oktoba 2021
Riba ya mkopo imepunguzwa kutoka 8.1% hadi 7.5% kwa mwaka kuanzia Januari 2022, na mwaka 2022 umetangazwa kuwa mwaka wa kuhamasisha akiba, amana na hisa.
MIKUTANO
Mafunzo kwa wawakilishi na watendaji wa URA SACCOS mkoani Mbeya
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Ulrich Matei, alifungua mafunzo hayo tarehe 27 Oktoba 2021 katika Hoteli ya Mbeya Highlands.
